C/O TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME, MABIBO ROAD,
P O BOX 8921, DAR ES SALAAM, TEL. +255 22 2443205;2443450;2443286
Mobile 255 754 784 050 Fax. 2443244, Email info@tgnp.org, web TGNP
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VISIINGILIE UCHAGUZI MKUU; KUVURUGA AMANI
1. Oktoba 1, 2010, Vyombo vya Ulinzi na Usalama; Makao Makuu ya Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Makao Makuu ya Jeshi ka Polisi
vilitoa tamko, kupitia Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, Mnadhimu
Mkuu wa JWTZ, juu ya ulinzi na usalama kuhusu amani wakati wa kampeni
na uchaguzi. Kesho yake, yaani Oktoba 2, vyombo vya habari nchini
vilikariri tamko hilo, na hivyo kusambaza ujumbe na maudhui yake kwa
wananchi na umma kwa ujumla, kama ilivyokusudiwa.
2. Katika ujumla wake, Tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama
linasisitiza umuhimu wa wadau wa uchaguzi kulinda amani na usalama,
ambazo ni tunu za Taifa la Tanzania, hususan katika kipindi hiki cha
kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010. Tamko linawakumbusha wadau wa
uchaguzi; wananchi, asasi za kiraia, mashirika ya dini na vyama vya
siasa, umuhimu wa kutunza na kuenzi amani sawia na kushirikiana na
vyombo vya usalama kulinda amani. Aidha wadau wanakumbushwa wajibu wa
majeshi; JWTZ na polisi kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kuwa katika
hali ya amani na usalama. Hili ni jambo jema kwa faida na ustawi wa
taifa letu ambalo wengi wa wananchi wake bado ni maskini sana.
3. Hata hivyo, licha ya Tamko kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa
kuenzi na kulinda amani na usalama wa taifa lao, sisi mashirika
yanayotetea Usawa wa Jinsia, Haki za Binadamu na Maendeleo na Ukombozi
wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct) tumeshitushwa, hatukubaliani na
tunalaani kwa jinsi na namna (mtindo) tamko la vyombo vya ulinzi na
usalama lilivyotolewa, uhalali wa wahusika kutoa tamko hilo, kipindi
lilipotolewa tamko hilo, mantiki yake, mwelekeo wa maudhui yake na
chombo kilichotoa tamko husika kwa sababu zifuatazo:
i). Tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama linakiuka, na ni kinyume cha
Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977. Ibara 138 haibainishi kuwa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama yatajihusisha moja kwa moja na masuala ya
Uchaguzi wala kubainisha kuwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani Rais wa Jamhuri,
anaweza kutoa amri kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama kuingilia shughuli
za Uchaguzi Mkuu, au chaguzi nyinginezo. Aidha ibara ya 74 ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano ya 1977, haitaji wala kutambua Majeshi ya
Ulinzi na Usalama kama sehemu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kitendo
cha Majeshi ya Ulinzi na Usalama kutoa tamko kupitia vyombo vya habari
ni dhahiri kinalenga kutoa vitisho, kuchochea, kuingilia mchakato, na
bila shaka kuvuruga Uchaguzi Mkuu unaokusudiwa kufanyika Oktoba 31. Na
kama hivyo ndivyo, WanaFemAct tunalazimika kuamini kuwa tamko la
vyombo vya Ulinzi na Usalama limeficha na kusheheneza malengo ya
maslahi binafsi, siyo maslahi ya nchi kama umma unavyoaminishwa.
ii). Hadi sasa, zaidi ya 'vijembe' vya hapa na pale baina ya wanasiasa
na vyama vya siasa vinavyoshindana na kujinadi kwa wananchi ili kupata
ridhaa ya kuongoza dola ya Tanzania, hakuna wala hakujatokea tishio
lolote la kuvurugika kwa amani. Vyama vya Siasa vimekuwa vikiendelea
kutangaza mipango ya sera zao, vijijini na mijini, kupitia mikutano ya
kampeni; wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuhudhuria mikutano
ya kampeni, kusikiliza na kuchambua ahadi mbalimbali zinazotolewa na
wanasiasa na vyama vyao; vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti taarifa
mbalimbali kuhusiana na mambo yanayojiri kwenye mikutano ya kampeni,
na hata kampeni za nyumba kwa nyumba; asasi za kiraia, kwa
kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, zimekuwa zikiendelea kutoa
elimu ya mpiga kura kwa makundi mabalimbali ya wapiga kura watarajiwa;
Msajili wa Vyama Vya siasa amekuwa akiendelea kufuatilia utekelezaji
wa Maadili ya Vyama vya Siasa Wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010 na Sheria
ya Gharama za Uchaguzi; na Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa
ikiendelea kuratibu kampeni, kusimamia manunuzi ya vifaa tayari kwa
kusambazwa katika vituo 52 000 vya kupigia kura nchini kote,
kuthibitisha usahihi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, na kuratibu
wadau wengine wa uchaguzi, kwa mfano, waangalizi wa ndani na nje wa
uchaguzi. Hayo yote yakiwa yanaendelea hakujatokea tishio la kuvurugwa
kwa amani wala tatizo la kiusalama. Kama hivi ndivyo, wanaFemAct
tunaendelea kuamini kuwa tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama lina
agenda yake; ya siri. Si bure! Litakuwa ni jambo la kushangaza na
kusikitisha sana iwapo Watanzania watabaini kuwa vyombo vyao vya
ulinzi na usalama vimeanza kutumiwa vibaya na wanasiasa na vyama vya
siasa kwa manufaa ya kikundi maslahi binafsi cha vatu wachache.
iii). Jeshi la Wananchi wa Tanzania halipaswi kujihusisha na masuala
ya ndani ya usalama wa raia. Kama kweli kungekuwa na tishio la amani
na usalama, basi tungetegemea kuona Jeshi la Polisi, chombo chenye
dhamana ya kuhakikisha kunakuwa na hali ya usalama kwa raia na mali
zao, likitoa tamko hilo; siyo JWTZ. Sasa kama hivyo ndivyo, wanaFemAct
tunasikitika na kushangaa kuona Jeshi la Wananchi wa Tanzania
likifanya kazi za polisi wakati askari wa Jeshi la Polisi wapo tele,
pamoja na Inspekta Jenerali wao. Hali hii haieleweki na ni kinyume cha
kanuni za msingi za utawala bora. Inakuwaje askari polisi waendelee
kulipwa mshahara wakati kazi zao zinafanywa na wanajeshi wa JWTZ!
iv). Ujumbe unaotolewa na tamko la Vyombo vya Usalama kuwa
"vimejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu, kikundi, chama au
taasisi yoyote... itakayochochea kuyakataa matokeo ya uchaguzi" ni
kitisho cha dhahiri, si kwa vyama vya siasa na wagombea pekee, bali
pia ni dhidi ya jitihada za kujenga na kuimarisha utawala bora na
demokrasia kwa ujumla hapa nchiniTanzania. Ni dhahiri Luteni Jenerali
Abdulhaman Shimbo anafahamu kuwa si wanajeshi wala silaha zinazoweza
kulazimisha wananchi, vyama vya siasa na wagombea wao wakubaliane na
matokeo ya uchaguzi bali uchaguzi unaokubalika miongoni mwa washindani
na wananchi kwa ujumla kuwa umefanyika kwa kuzingatia vigezo vya
msingi vya chaguzi huru na haki. Katika kutimiza hili, usimamizi imara
na usiokuwa na upendeleo, na vyombo vya usalama na vyombo vya habari
visivyopendelea upande wowote ni nguzo muhimu kuhakikisha washindani
wa kisiasa wanakubaliana na matokeo ya uchaguzi. Yaliyotokea katika
nchi za Romania, Ukraine, Zimbabwe, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Burundi na kwingineko duniani ni mifano inayotoa mafunzo ya
kutosha kwa raia na wanajeshi pia. Hakika hili halihitaji tamko la
Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Kama hivyo ndivyo, wanaFemAct hatuoni
sababu iliyopelekea Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoa tamko lake, na
hasa katika kipindi hiki ambacho kampeni zinaendelea vizuri. FemAct
hatuko tayari kuona Tanzania inapitishwa ya machafuko ya kupandikiza
kwa lengo la kunufaisha kirundi maslahi cha vatu wachache.
Kwa kuzingatia sababu zetu hapo juu, wanaFemAct tunapendekeza
ifuatavyo:
a). Vyombo vya Ulinzi na Usalama viache mara moja kuingilia mchakato
wa uchaguzi kwa kuwa jambo hili linaweza kusabaisha vitisho na vurugu
dhidi ya wapiga kura na wananchi kwa ujumla; kuchafua hali ya amani na
usalama ambayo ni tunu ya Tanzania. Lakini iwapo kutakuwa na haja ya
kufanya hivyo, basi sheria husika sharti zifuatwe, Jeshi la Polisi
likiwa na dhamana ya kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
b). Wanasiasa, vyama vya siasa na viongozi waache mara moja
kujitafutia ushindi kwa kutumia mlango wa nyuma. Uongozi wa dola
sharti upatikane kupitia mashindano ya wazi kusaka ridhaa ya wananchi
kidemokrasia katika uchaguzi unaokubalika kuwa huru na haki, siyo
kutumia vyombo vya Ulinzi na Usalama kutisha wapiga kura ili
kujihakikishia ushindi.
c). Vyombo vya habari viendelee kuhabarisha wananchi na wapiga kura
juu ya mipango ya sera za vyama vya siasa na ahadi za wagombea kama
inavyojiri katika mikutano ya kampeni.
d). Asasi za kiraia ziendelee kuelimisha wananchi juu masuala
mbalimbali yanayoongeza uangavu kwa wapiga kura, na wananchi kwa
ujumla juu ya sheria, taratibu, kanuni za uchaguzi, haki na wajibu wa
kuhudhuria mikutano ya kampeni, kusikiliza ahadi za wagombea, kufanya
maamuzi na hatimaye kujitokeza kupiga kura.
e). Wapiga kura waendelee kujibidisha kupata elimu ya mpiga kura,
kuhudhuria mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na wagombea, na
kusikiliza kwa makini ahadi za wagombea wakipembua na kuchambua kati
ya pumba na mchele ili kunako Oktoba 31 wafanye uamuzi kwa kihistoria
kuchagua viongozi watakaoweza kushirikiana na wananchi kukwamua Taifa
letu kuondokana na umaskini na kuletea Taifa heshima.
Mwisho/
FemAct
Dar es Salaam, Oktoba 6, 2010.

Kwa habari zaidi tembelea,
No comments:
Post a Comment