soma makala hii ya Dr.Kitilla Mkumbo wa UDSM
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=20153
Wednesday, 13 October 2010
Friday, 8 October 2010
saratani ya ngozi kwa albino ni janga la taifa
http://www.mwananchi.co.tz/makala/-/5357-saada-saratani-inakula-uso-wangu
Na Florence Majani.gazeti Mwananchi Oct 7, 2010
MSISIMKO wa ajabu lazima ukukumbe pale utakapokutana naye akiwa na kidonda kilichosababisha shimo katika mwamba wa pua yake. Huku juu ya shavu lake la kulia kuna kovu la kidonda nacho kikiwa kimetengeneza shimo na kuufanya uso wake uwe wa kustaajabisha.
Saada Rashid amezaliwa Ifakara, Morogoro, miaka 30 iliyopita akiwa ni binti pekee kwa wazazi wake. Amezaliwa na ulemavu wa ngozi huku akitoka katika familia yenye kipato duni, hivyo maisha yake kuwa ya kubahatisha kila kunapokucha.
Anasema, kwa bahati mbaya mama yake alifariki mwaka 2005, na kwa sababu asingeweza kuishi kwa mama wa kambo ilimbidi akaishi kwa shangazi yake na huko hali haikuwa shwari.
“Shangazi yangu naye hakuwa na maisha mazuri, tulikuwa na maisha ya tabu, baya zaidi mjomba wangu alikuwa hanitaki na alipenda kulalamika sana. Maneno yake ya chinichini yalizidi baada ya mimi kupata ujauzito. Mjomba alidiriki kumtamkia shangazi kuwa hanitaki kama nisingeondoka basi angemfukuza hata na shangazi,”anasema Saada
Kwa bahati mbaya Saada alipachikwa ujauzito huo na mume wa mtu, ambaye mbali na kuwa na watoto, pia hana shughuli yoyote ya kumuingizia kipato.
Maisha ya Saada yalikuwa hatarini na hakuwa na muelekeo baada ya shangazi yake kuitii amri ya mjomba wake na kumfukuza.
“Nilipojifungua tu ndipo nilipofukuzwa rasmi nyumbani kwa shangazi yangu, nikaamua kujitafutia mahali pa kuishi, sikuwa na ndugu yoyote, nikachukua uamuzi wa kwenda katika nyumba ya masista, kituo cha masista cha kulea watu wenye ukoma. Nikaomba wanipe msaada mimi na mwanangu kwa bahati nzuri nilimkuta sista mmoja, Maria Paulo huyo alinionea huruma na akanisaidia nikaanza rasmi kuishi katika kituo hicho,” anasema Saada.
Hakupenda kuishi katika kituo kile, alitamani ajitegemee na amlee mtoto wake wa kike aliyempa jina la Swaiba. Akamuomba sista Maria ampe fedha za kujikimu akaanze maisha kijijini kwao Ifakara.
“Nikamuomba sista Maria anipe msaada ili nikatafute kiwanja nianze maisha ya kujitegemea, akaniambia anao uwezo wa kunipa shilingi laki nne tu na akasema hana fedha zaidi ya hizo. Nikasaidiwa kupata kiasi hicho cha fedha nikaenda kijijini kwetu nikanunua kiwanja kwa shilingi 70,000, na kisha nikajenga nyumba ya matofali ya kuchoma, nikawa nalima napata chakula kidogo,”anasema.
Baada ya muda akaanza kuona kidonda kidogo katika paji lake la uso, akaenda hospitali ya Ifakara akatibiwa kwa kutiwa dawa na kufungwa lakini kidonda kile hakikupona kabisa na ndipo alipopewa barua ya kwenda hospitali ya taifa ya Muhimbili.
“Pale Muhimbili nikafanyiwa vipimo madaktari wakasema haikuwa kansa ni vidonda vya kawaida nikapewa dawa za kunywa na kupaka nikarudi Ifakara lakini kidonda kile hakikupata nafuu yoyote nikaenda tena Muhimbili.
Safari hii nikakwanguliwa nyama ya paji la uso pale kwenye kidonda halafu wakanikata nyama katika paja langu la kulia na kuziba shimo la kwenye uso,”anaelezea Saada.
Hata hivyo amani ya Saada haikudumu kwa muda mrefu kwani October 2008, kikaanza kidonda kipya, safari hii kikiwa juu kidogo ya sikio. Hata hivyo hakuweza kufanya lolote kwa sababu hakuwa na fedha hata za kula yeye na mtoto wake na kipindi hicho alikuwa amebeba ujauzito wa pili.
“Nikashindwa kwenda hospitali sikuwa na fedha kabisa, nikaamua kwenda kwa shangazi yangu kumuomba msaada kwani kidonda kilikuwa kinaniuma na sikuwa nikilala usiku isitoshe nilikuwa nina ujauzito wa mtoto huyu. Watoto wa shangazi wakachanga shilingi elfu tano tano kila mmoja wakanipa niende hospitali,”anaeleza.
Kile alichokitegemea hospitali ya Ifakara sicho alichokipata, kwani baada ya madaktari kumpima wakashauri akatwe sehemu ya nyama yake ili ikapimwe Ulaya na hapo alitakiwa atoe shilingi 30,000.
“Sikuwa na fedha hizo ndipo wakaniambia niende Ocean Road, wakaniambia nisubiri barua, niliisubiri kwa miezi mitatu hadi Desemba 2009 ndipo nilipopewa na kuipeleka Ocean Road, sikuwa na nauli. Nikaamua kumtafuta yule sista Maria aliyenisaidia kipindi kile nikaenda katika kituo alichokuwa akikaa kwa bahati mbaya nikaambiwa mtu huyo alikwisharudi Ulaya. Nilikosa nguvu nikakata tamaa, nikajikaza na kuwaelezea matatizo yangu nikawaambia sipajui Dar es Salaam wala sina ndugu wakanipa 20,000,”anasema Saada.
Nauli ya kutoka Ifakara kwenda Dar es Salaam, ilikuwa ni shilingi 20,000 hivyo mkononi mwake alikuwa na kiasi hicho tu bila akiba ya matumizi mengine akiwa na mtoto mdogo wa miezi mitano mgongoni mwake.
“Ikanibidi nitafute mtu wa kumuachia mtoto yaani Swahiba nikamuacha kwa shangazi yangu. Kwa bahati nzuri nikiwa katika gari nikakutana na msamaria mwema, mama Shukuru ambaye alinipa msaada mkubwa. Nilipofika hapa Dar es Salaam nikafikia nyumbani kwake Yombo. Asubuhi siku iliyofuata akanileta hapa Ocean Road,”anasimulia Saada.
Alipofika Ocean Road madaktari wa pale walimwambia aende Muhimbili akachukue kwanza vipimo ili wavifanyie kazi. Hatua za uchukuaji wa vipimo hivyo haukuwa wa siku moja na ilimbidi apewe kitanda lakini hilo halikuwezekana.
“Muhimbili walikataa mimi kulazwa nikiwa na mtoto wa miezi mitano, ikanibidi nikae kwa mama Shukuru huku nikiendelea kufanya vipimo nikawa nasaidiwa nauli na jirani mwingine kwa sababu hata mwenyeji wangu hakuwa na uwezo wa kunipa nauli ya kila siku,” anasema Saada.
Anasema, machi 23 mwaka huu akafanikiwa kupelekwa Ocean Road akagundulika kuwa saratani inamla sehemu za usoni na kwenye ubongo. Ndipo madaktari wakaamua aanzishiwe tiba ya mionzi.
“Nikaanza na tiba ya mionzi, nikapigwa mionzi 10 mara ya kwanza na mara ya pili nikapigwa mionzi saba nikaruhusiwa na kuambiwa nirudi tena Septemba 15,”anaeleza.
Kabla ya tarehe ya kurudi kiliniki kikaanza kidonda cha puani, kila alipoenda kukitibu hospitali hakikupona, ndipo alipoamua kutafuta nauli na alipopata alipanda treni na kuja Dar es Salaam.
“Nilifikia tena kwa mama Shukuru, nikapewa kitanda hapa Ocean Road nikaanza matibabu nikakatwa tena nyama hapa puani na nikaendelea na tiba ya mionzi,”anasema.
Pamoja na kuugulia maumivu makali yasababishwayo na saratani inayomla katika uso wake, inambidi Saada akae na mtoto wake mdogo mwenye mwaka mmoja hospitalini hapo. Uso wake unaendelea kumegwa siku hadi siku kwa sababu kansa hiyo ipo mwilini mwake, hana msaada wa kifedha kwake na mtoto wake.
Kwa huzuni huku machozi yakimtoka Saada anasema, “Sikupenda kuwa hivi, napata mateso makali sana. Natamani kupona, natamani kufanya kazi lakini sijasoma nimekomea darasa la nne hata hivyo naweza kufanya kitu cha kuniingizia fedha kwa kukodi shamba na kutafuta vibarua watakaolima, kwa sababu nimeambiwa nisikae juani”.
Leo ni Saada na kesho ni wewe, mzazi wako au ndugu yako haya humkuta kila mtu mwenye pumzi bila kupanga wala kupenda. Maisha yake ni ya taabu anahitaji msaada wako kwani hakupenda kuwa mlemavu na wala hakuombea saratani hii imtafune usoni.
Kwa yeyote ambaye anapenda kumsaidia anaweza kuwasiliana na mwandishi wa makala haya 0715773366

Thursday, 7 October 2010
TAMKO LA FEMACT KUHUSU KAULI YA JWTZ JUU YA UCHAGUZI
C/O TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME, MABIBO ROAD,
P O BOX 8921, DAR ES SALAAM, TEL. +255 22 2443205;2443450;2443286
Mobile 255 754 784 050 Fax. 2443244, Email info@tgnp.org, web TGNP
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VISIINGILIE UCHAGUZI MKUU; KUVURUGA AMANI
1. Oktoba 1, 2010, Vyombo vya Ulinzi na Usalama; Makao Makuu ya Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Makao Makuu ya Jeshi ka Polisi
vilitoa tamko, kupitia Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, Mnadhimu
Mkuu wa JWTZ, juu ya ulinzi na usalama kuhusu amani wakati wa kampeni
na uchaguzi. Kesho yake, yaani Oktoba 2, vyombo vya habari nchini
vilikariri tamko hilo, na hivyo kusambaza ujumbe na maudhui yake kwa
wananchi na umma kwa ujumla, kama ilivyokusudiwa.
2. Katika ujumla wake, Tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama
linasisitiza umuhimu wa wadau wa uchaguzi kulinda amani na usalama,
ambazo ni tunu za Taifa la Tanzania, hususan katika kipindi hiki cha
kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010. Tamko linawakumbusha wadau wa
uchaguzi; wananchi, asasi za kiraia, mashirika ya dini na vyama vya
siasa, umuhimu wa kutunza na kuenzi amani sawia na kushirikiana na
vyombo vya usalama kulinda amani. Aidha wadau wanakumbushwa wajibu wa
majeshi; JWTZ na polisi kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kuwa katika
hali ya amani na usalama. Hili ni jambo jema kwa faida na ustawi wa
taifa letu ambalo wengi wa wananchi wake bado ni maskini sana.
3. Hata hivyo, licha ya Tamko kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa
kuenzi na kulinda amani na usalama wa taifa lao, sisi mashirika
yanayotetea Usawa wa Jinsia, Haki za Binadamu na Maendeleo na Ukombozi
wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct) tumeshitushwa, hatukubaliani na
tunalaani kwa jinsi na namna (mtindo) tamko la vyombo vya ulinzi na
usalama lilivyotolewa, uhalali wa wahusika kutoa tamko hilo, kipindi
lilipotolewa tamko hilo, mantiki yake, mwelekeo wa maudhui yake na
chombo kilichotoa tamko husika kwa sababu zifuatazo:
i). Tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama linakiuka, na ni kinyume cha
Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977. Ibara 138 haibainishi kuwa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama yatajihusisha moja kwa moja na masuala ya
Uchaguzi wala kubainisha kuwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani Rais wa Jamhuri,
anaweza kutoa amri kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama kuingilia shughuli
za Uchaguzi Mkuu, au chaguzi nyinginezo. Aidha ibara ya 74 ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano ya 1977, haitaji wala kutambua Majeshi ya
Ulinzi na Usalama kama sehemu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kitendo
cha Majeshi ya Ulinzi na Usalama kutoa tamko kupitia vyombo vya habari
ni dhahiri kinalenga kutoa vitisho, kuchochea, kuingilia mchakato, na
bila shaka kuvuruga Uchaguzi Mkuu unaokusudiwa kufanyika Oktoba 31. Na
kama hivyo ndivyo, WanaFemAct tunalazimika kuamini kuwa tamko la
vyombo vya Ulinzi na Usalama limeficha na kusheheneza malengo ya
maslahi binafsi, siyo maslahi ya nchi kama umma unavyoaminishwa.
ii). Hadi sasa, zaidi ya 'vijembe' vya hapa na pale baina ya wanasiasa
na vyama vya siasa vinavyoshindana na kujinadi kwa wananchi ili kupata
ridhaa ya kuongoza dola ya Tanzania, hakuna wala hakujatokea tishio
lolote la kuvurugika kwa amani. Vyama vya Siasa vimekuwa vikiendelea
kutangaza mipango ya sera zao, vijijini na mijini, kupitia mikutano ya
kampeni; wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuhudhuria mikutano
ya kampeni, kusikiliza na kuchambua ahadi mbalimbali zinazotolewa na
wanasiasa na vyama vyao; vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti taarifa
mbalimbali kuhusiana na mambo yanayojiri kwenye mikutano ya kampeni,
na hata kampeni za nyumba kwa nyumba; asasi za kiraia, kwa
kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, zimekuwa zikiendelea kutoa
elimu ya mpiga kura kwa makundi mabalimbali ya wapiga kura watarajiwa;
Msajili wa Vyama Vya siasa amekuwa akiendelea kufuatilia utekelezaji
wa Maadili ya Vyama vya Siasa Wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010 na Sheria
ya Gharama za Uchaguzi; na Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa
ikiendelea kuratibu kampeni, kusimamia manunuzi ya vifaa tayari kwa
kusambazwa katika vituo 52 000 vya kupigia kura nchini kote,
kuthibitisha usahihi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, na kuratibu
wadau wengine wa uchaguzi, kwa mfano, waangalizi wa ndani na nje wa
uchaguzi. Hayo yote yakiwa yanaendelea hakujatokea tishio la kuvurugwa
kwa amani wala tatizo la kiusalama. Kama hivi ndivyo, wanaFemAct
tunaendelea kuamini kuwa tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama lina
agenda yake; ya siri. Si bure! Litakuwa ni jambo la kushangaza na
kusikitisha sana iwapo Watanzania watabaini kuwa vyombo vyao vya
ulinzi na usalama vimeanza kutumiwa vibaya na wanasiasa na vyama vya
siasa kwa manufaa ya kikundi maslahi binafsi cha vatu wachache.
iii). Jeshi la Wananchi wa Tanzania halipaswi kujihusisha na masuala
ya ndani ya usalama wa raia. Kama kweli kungekuwa na tishio la amani
na usalama, basi tungetegemea kuona Jeshi la Polisi, chombo chenye
dhamana ya kuhakikisha kunakuwa na hali ya usalama kwa raia na mali
zao, likitoa tamko hilo; siyo JWTZ. Sasa kama hivyo ndivyo, wanaFemAct
tunasikitika na kushangaa kuona Jeshi la Wananchi wa Tanzania
likifanya kazi za polisi wakati askari wa Jeshi la Polisi wapo tele,
pamoja na Inspekta Jenerali wao. Hali hii haieleweki na ni kinyume cha
kanuni za msingi za utawala bora. Inakuwaje askari polisi waendelee
kulipwa mshahara wakati kazi zao zinafanywa na wanajeshi wa JWTZ!
iv). Ujumbe unaotolewa na tamko la Vyombo vya Usalama kuwa
"vimejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu, kikundi, chama au
taasisi yoyote... itakayochochea kuyakataa matokeo ya uchaguzi" ni
kitisho cha dhahiri, si kwa vyama vya siasa na wagombea pekee, bali
pia ni dhidi ya jitihada za kujenga na kuimarisha utawala bora na
demokrasia kwa ujumla hapa nchiniTanzania. Ni dhahiri Luteni Jenerali
Abdulhaman Shimbo anafahamu kuwa si wanajeshi wala silaha zinazoweza
kulazimisha wananchi, vyama vya siasa na wagombea wao wakubaliane na
matokeo ya uchaguzi bali uchaguzi unaokubalika miongoni mwa washindani
na wananchi kwa ujumla kuwa umefanyika kwa kuzingatia vigezo vya
msingi vya chaguzi huru na haki. Katika kutimiza hili, usimamizi imara
na usiokuwa na upendeleo, na vyombo vya usalama na vyombo vya habari
visivyopendelea upande wowote ni nguzo muhimu kuhakikisha washindani
wa kisiasa wanakubaliana na matokeo ya uchaguzi. Yaliyotokea katika
nchi za Romania, Ukraine, Zimbabwe, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Burundi na kwingineko duniani ni mifano inayotoa mafunzo ya
kutosha kwa raia na wanajeshi pia. Hakika hili halihitaji tamko la
Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Kama hivyo ndivyo, wanaFemAct hatuoni
sababu iliyopelekea Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoa tamko lake, na
hasa katika kipindi hiki ambacho kampeni zinaendelea vizuri. FemAct
hatuko tayari kuona Tanzania inapitishwa ya machafuko ya kupandikiza
kwa lengo la kunufaisha kirundi maslahi cha vatu wachache.
Kwa kuzingatia sababu zetu hapo juu, wanaFemAct tunapendekeza
ifuatavyo:
a). Vyombo vya Ulinzi na Usalama viache mara moja kuingilia mchakato
wa uchaguzi kwa kuwa jambo hili linaweza kusabaisha vitisho na vurugu
dhidi ya wapiga kura na wananchi kwa ujumla; kuchafua hali ya amani na
usalama ambayo ni tunu ya Tanzania. Lakini iwapo kutakuwa na haja ya
kufanya hivyo, basi sheria husika sharti zifuatwe, Jeshi la Polisi
likiwa na dhamana ya kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
b). Wanasiasa, vyama vya siasa na viongozi waache mara moja
kujitafutia ushindi kwa kutumia mlango wa nyuma. Uongozi wa dola
sharti upatikane kupitia mashindano ya wazi kusaka ridhaa ya wananchi
kidemokrasia katika uchaguzi unaokubalika kuwa huru na haki, siyo
kutumia vyombo vya Ulinzi na Usalama kutisha wapiga kura ili
kujihakikishia ushindi.
c). Vyombo vya habari viendelee kuhabarisha wananchi na wapiga kura
juu ya mipango ya sera za vyama vya siasa na ahadi za wagombea kama
inavyojiri katika mikutano ya kampeni.
d). Asasi za kiraia ziendelee kuelimisha wananchi juu masuala
mbalimbali yanayoongeza uangavu kwa wapiga kura, na wananchi kwa
ujumla juu ya sheria, taratibu, kanuni za uchaguzi, haki na wajibu wa
kuhudhuria mikutano ya kampeni, kusikiliza ahadi za wagombea, kufanya
maamuzi na hatimaye kujitokeza kupiga kura.
e). Wapiga kura waendelee kujibidisha kupata elimu ya mpiga kura,
kuhudhuria mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na wagombea, na
kusikiliza kwa makini ahadi za wagombea wakipembua na kuchambua kati
ya pumba na mchele ili kunako Oktoba 31 wafanye uamuzi kwa kihistoria
kuchagua viongozi watakaoweza kushirikiana na wananchi kukwamua Taifa
letu kuondokana na umaskini na kuletea Taifa heshima.
Mwisho/
FemAct
Dar es Salaam, Oktoba 6, 2010.

Kwa habari zaidi tembelea,
Subscribe to:
Posts (Atom)